Home » Uncategories » Hii ni laana Kubwa,Mtu Na Dadaye Wafumaniwa Wakifanya mapenzi, Kaka mtu auawa kinyama na shemeji yake, Dada mtu apasuliwa utumbo nje.
Hii ni laana Kubwa,Mtu Na Dadaye Wafumaniwa Wakifanya mapenzi, Kaka mtu auawa kinyama na shemeji yake, Dada mtu apasuliwa utumbo nje.
Mwenye mali' amchinja kaka, dada apasuliwa tumbo, utumbo nje!
"ALIMCHUKULIA kama shemeji, akamwamini kumbe kaka mtu alikuwa akishughulika ipasavyo na dada yake. Ilibaki siri nzito mpaka alipogundua mwaka huu na kufanya mauaji ya kutisha..."
Hivi ndivyo alivyoanza kusimulia mdogo wa marehemu Juma Matimbwa, Salum Shemtumba alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Kimara Machungwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Mazengo kumuua kwa kisu, Juma Matimbwa na kumjerui vibaya hawara yake Angelina Michael, baada ya kuwafumania wakiwa wanavunja amri ya sita ya Mungu.
Akielezea sakata zima Shemtumba, alisema tukio hilo lilitokea Mei 15, mwaka huu maeneo ya Kimara King’oko baada ya Mazengo kupata habari kuwa shemeji yake Juma ana uhusiano na dada yake ambaye ndiye mpenzi wake.
Mtoa habari wetu huyo alizidi kuweka wazi kuwa baada ya kupata habari hiyo kutoka kwa watu wa karibu, akaanza kuzifuatilia kwa kina kama zina ukweli wowote huku akiandaa mtego wa kuwakamata mtu na dada yake ambao ni binamu ili kuweza kujua ukweli.
ALIVYOWAFUMA
Shemtumba alisema siku hiyo ya tukio Mazengo alifanikiwa kuwakuta chumbani Juma na Angelina baada ya kupata taarifa saa 6 mchana kutoka kwa wapambe kuwa shemeji yake huyo alifika nyumbani hapo na kuendelea kujivinjari na mpenzi wake(dada mtu).
“Kabla hajafika alikwenda nyumbani kwake ambako alichukua kisu na kuja kuwavamia,” alidai Shemtumba.
Aliongeza kuwa baada ya kuwafumania alianza kumkata sehemu mbalimbali za mwili Juma (marehemu) huku akimshambulia mpenzi wake kwa kisu tumboni na kichwani.
Aliendelea kusema kuwa baada ya Angelina kuona anashambuliwa, aliamua kukimbia na kujificha huku damu zikimtoka kwa wingi mpaka watu walipokuja sehemu ya tukio na kuanza kuamulia ugomvi huo ambapo Juma alikuwa ameshafariki kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kukatwakatwa kwa kisu mwilini na Mazengo alielekea kituo cha polisi kujisalimisha.
“ Baada ya Mazengo kufanya mauaji tu alienda kujisalimisha mwenyewe Kituo cha Polisi cha Kimara ambapo askari waliamua kumhamishia kituo kikubwa cha Mbezi kwa Yusufu,” alisema.
ANGELINA ASIMULIA
Gazeti hili lilienda mpaka nyumbani kwa Angelina ambapo lilimkuta ndiyo anatoka Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa na akajitetea kuwa yeye hakuwa na uhusiano na Juma kwa vile ni kaka yake na alikuja pale kwa lengo la kumsalimia tu na si vinginevyo.
Angelina aliongeza kuwa siku ya tukio alikuwa na kaka yake hapo nyumbani kwake kwa kuwa anauza pombe za kienyeji na kaka huyo alikuwa akinywa.
Baada ya muda mfupi waliongozana hadi kwenye kibanda cha Tigo Pesa kw ajili ya kuchukua fedha ili amlipe baada ya kupata kinywaji.
Aliendelea kusema kuwa baada ya kurudi nyumbani alikuja Mazengo na kuanza kutukana bila kujua alikuwa na kisu na kuanza kuwachoma na kufanikiwa kumuua kaka yake kisha kumgeukia yeye na kumchoma tumboni.
Alisema aliamua kukimbia nje ili kujinusuru maisha yake.
“ Mimi kwa kweli namshangaa sana Mazengo kwa kuwa sikuwa na uhusiano wowote na marehemu Juma kwa vile alikuwa ni kaka yangu kabisa na mara nyingi alikuwa akija nyumbani kwangu na yeye alikuwa akimfahamu,” alisema Angelina akiwa katika maumivu makali
Posted