Latest Updates

IYOBO: HATA KAMA AUNT AMENIZIDI UMRI, HAIHUSU




Dansa grade one wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Iyobo akiwa na Aunt Ezekiel.

DANSA grade one wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Moses Iyobo amenyanyua kinywa chake na kusema hata kama mpenzi wake, Aunt Ezekiel amemzidi umri, ataendelea kumpenda hivyohivyo.
Akizungumza na mwanahabari wetu juzikati, Iyobo.

alisema watu wengi wamekuwa wakihoji yeye kumpenda Aunt
ambaye ana umri wa miaka 29, hawajui tu mapenzi hayaangalii umri kwani miaka ni namba tu za kuhesabika.
“Age is just a number, mimi sioni tatizo kuwa na Aunt. Nategemeaanizalie, awe mama wa watoto wangu. Kuhusu wale wanaosema nina mke mwingine, si kweli yule nilizaa naye tu lakini kwa Aunt ndiyo nimefika,” alisema Iyobo ambaye ana umri wa miaka 23.