Kingine ambacho amekisema Zitto Kabwe kwenye sentensi hizi SABA..
Leo ni siku ya tatu, kwenye siasa Tanzania kuna story kubwa ambayo bado inaendelea kuchukua Headlines kubwa, ni ishu ya Uongozi wa CHADEMA kutangaza kumsimamisha Uanachama Mbunge Zitto Kabwe.
Jana na leo Magazetini na kwenye vyombo vya habari kuna taarifa ya kingine alichokisema Mbunge huyo kuhusu taarifa za kusimamishwa uanachama; “Mimi ninaendelea na kazi kama hakuna kilichotokea.. Sina taarifa rasmi ya chochote ambacho kimetokea ndio maana ninaendelea na kazi.. Maamuzi yoyote ambayo yanatokea ni process. Hata ikiwa kwa mfano maamuzi ya chama ni kama ilivyotangazwa kuna process ya kuandika barua kwa Spika.. Spika kujiridhisha..
Minutes za vikao kwa sababu maamuzi yote ni lazima yafanywe na vikao sio mtu mmoja.. then Spika ananiandikia mimi… Kama nyinyi mnavyosikia kwenye vyombo vya habari na mimi hivyi hivyo nasikia… siwezi kujibizana na Chama changu“– Zitto Kabwe
Posted