Home » Uncategories » Michael Jordan anaingiza dola milioni 100 kila mwaka, fahamu zinakotoka soma hapa.
Michael Jordan anaingiza dola milioni 100 kila mwaka, fahamu zinakotoka soma hapa.
Mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu, Michael Jordan aliingiza dola milioni 100 kutoka kwa Nike na washirika wengine mwaka jana kwa mujibu wa mtandao wa Forbes, kuliko mwanamichezo yeyote aliyestaafu.
Pesa aliyoingiza mwaka jana, ni zaidi ya dola milioni 90 ya mshahara aliolipwa kwenye kipindi cha miaka 15 aliyochezea kwenye timu za Chicago Bulls na Washington Wizards.
Brand yake ya Jordan kupitia kampuni ya Nike ni mashine ya kuingiza fedha. Mauzo ya viatu vya Jordan nchini Marekani yalipanda mwaka jana kwa asilimia 17 kwa kufikia dola bilioni 2.6 kwa mujibu wa data zilizokusanywa na SportScanInfo.
Jordan anauza mara 10 zaidi ya viatu vya wachezaji wanaoendelea na kikapu akiwemo LeBron James. Kimataifa brand yake inaongeza dola bilioni 1 pia.
Brand ya Jordan ilishikilia asilimia 58 ya soko la viatu vya mpira wa kikapu mwaka jana kutoka asilimia 54% mwaka 2013.
Posted