Latest Updates

Picha: Ajali mbaya ya lori na basi yaua wengi Mafinga, abiria wapondwa na kontena



Zaidi ya watu 40 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 25 kujeruhiwa vibaya, kufuatia ajali mbaya iliyokea Jumatano hii maeneo ya Mafinga mkoani Iringa katika kijiji cha Changarawe baada ya lori la mizigo lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara, kugongana na gari la abiria la kampuni ya Majinja lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar es Salaam, kwa mujibu wa maelezo ya trafiki aliyekuwepo kwenye eneo la ajali.



Kontena la lori hilo liliilalia basi hiyo na watu wengine kupondwa huku wengine wakiporomokea kwenye korongo.



“Kuna watoto wawili hapa, makadirio ya miaka ni mitatu na saba, lakini hawa inasemekana kwamba walirushwa korongoni kutokana na huo mgongano,” ilisema taarifa kwenye mtandao wa Jamii Forums.



Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali katika eneo la tukio ulizorota kutokana na ukosefu wa gesi ya kukata basi kukosekana Mafinga.

Barabara ya kutoka Mbeya kabla ya kufika Mafinga ilifungwa kupisha zoezi la uokoaji.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kutokana na picha hizi

Vyanzo: Jamii Forums na EATV