Mastaa mbalimbali waliozungumza na Ijumaa Wikienda wakiongozwa na Wema Isaac Sepetu, walimponda na kumshangaa Aunt ambaye awali alikuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akimuunga mkono mgombea wake wa urais, Dk. John Pombe Magufuli ‘JM’.
“Yaani Aunt ametushangaza kwani alikuwa Team Magufuli. Ameonesha ni kiasi gani ni kigeugeu, sisi tunatarajia ushindi kwa asilimia kubwa. Sisi tumezaliwa na kukulia CCM hivyo hatuwezi kusaliti,” alisema Wema kwa niaba ya wenzake walipokuwa wakitangaza kuzindua kampeni za CCM zilizoanza jana. Jitihaza za kumpata Aunt hazikuzaa matunda.