Home » Uncategories » Harrison Mwakyembe Adai Mgombea Urais Edward Lowassa Alihusika Kwenye Ufisadi wa Richmond
Harrison Mwakyembe Adai Mgombea Urais Edward Lowassa Alihusika Kwenye Ufisadi wa Richmond
Mhe Mwakyembe amkaanga Lowassa kuhusu kadhia ya Richmond na kusema kuwa asikwepe maana tume ya Bunge ilimkuta na hatia na ikabidi ajiuzulu Uwaziri Mkuu.
Ameeleza hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kupitia CCM Mhe JPM leo huko Kyela katika mfululizo wa kampeni za mgombea huyo. Mhe Mwakyembe kaeleza kadhia hiyo kwa maelfu ya wananchi waliokuwa wakishangilia tangu mwanzo hadi mwisho na wameahidi na kuapa kutotoa kura zao kwa Lowassa!
Alieleza kuwa leo waTanzania wanalipia umeme kwa bei ya juu kutokana na uroho wa Fisadi huyo kwavile Tanesco iliingizwa kwenye mkataba mbovu na pia gharama za mabilioni zilizolipwa kufuatia mkataba mbovu na kesi zilizojiri baada ya mkataba kusitishwa!
Wakati huo huo aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe Mwakipesile, aliyestaafu ameuambia mkutano huo kuwa yeye hawezi kukihama chama cha Mapinduzi kilichomsomesha na kukulia kama mwanachama.
Hii inavunja uongo uliozushwa dhidi yake kuwa kakihama chama hicho na kuhamia UKAWA!
Posted