Latest Updates

Nimekusogezea Hapa Kauli ya Mkapa, Lowassa na style mpya ya kampeni, + Hofu ya mvua za El Nino DAR. (Audio)






Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita? Jukumu langu ni kuhakikisha zile zote zinazoweka headlines magazetini kila asubuhi zinakufikia…

Mgombea Urais kupitia CHADEMA Edward Lowassa aanza kampeni kwa style ya kipekee kwa kupanda daladala kwa nia ya kusikiliza kero zinazowakabili madereva na makondakta kwenye usafiri wa uma… Mgombea Urais kupitia CCM John Magufuliasema kwenye safari yake ya kampeni atatumia usafiri wa barabara ili kuzijua kero za wananchi kwa ukaribu.

Kauli ya Benjamin Mkapa yazua mjadala, Rais za Zanzibar Dk. Ali Mohammed Sheinachukua fomu ya ugombea Urais kupitia Chama Cha CCM, NEC yawashukiaCHADEMA... Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrence Mashaakamatwa na kuwekwa rumande baada ya kujaribu kuwawekea dhamana vijana 17 wajulikanao kama 4U Movement.

Hali ya Kipindupindu jijini Dar es salaam yazidi kuwa tete idadi ya wagonjwa yafika 83kwa wilaya za Temeke na Ilala… Mkurugenzi wa mamlaka ya hali wa hewa nchini asema nchi za Africa Mashariki zipo kwenye hati hati ya kukumbwa na mvua kubwa za El Ninomiezi ya September mpaka December kutokana na joto kubwa.

Sauti yote ya uchambuzi wa magazeti kupitia #PowerBreakfast nimeisogeza kwako hapa chini.