BAADA ya Waziri wa Maliasili na Utanii Balozi Khamis Kaghasheki
kujiuzuru, Waziri Mkuu Mizengo Pinda pia alifikia hatua ya kujiuzuru kwa
staili ya kusubiri uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye yuko nchini
Marekani kwa uchunguzi wa Afya yake, hatua ya mawaziri kuwajibika
inatokana na vitendo vya mauaji ya wananchi na mifugo yao pamoja na
manyanyaso makubwa, zilizofanywa na Wanajeshi wa Tanzania wakati wa
Operesheni Tokomeza Ujangili, kwakuwa yeye ndiye msimamizi wa shughuli
zote za serikali.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia),(kushoto) Askari wa Jeshi la Polisi ikitekeleza majuku yao
Mbali na Waziri Mkuu mawaziri
wengine waliokumbwa na kashfa hiyo na kulazimishwa kujiuzuru ni pamoja
na Waziri wa Mambo ya Ndani na nchi (Dk Emmanuel Nchimbi), Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (Shamsi Vuai Nohodha)na Waziri wa Uvuvi
na Mifugo (Mathayo David Mathayo).
"Nimezungumza na
mawaziri,nimezungumza na mkuu wa nchi, kuhusu hali ilivyo
nchini,mawaziri wamekubali kuwajibika na Rais Kikwete amebariki uamuzi
wao"alisema Pinda.