
Anachokisema akitaka watu wamuelewe ni kwamba: "Ney ni kaka yangu, Ney ni mshkaji na hakuna msanii anaeingia na kutoka kwangu kama yeye, nilichopost kuhusu maoni yangu juu ya wimbo wake ni utani."
Ni blog ndogondogo waliichukua post yangu na kuripoti kwamba nimemdiss ila hakuna kibaya chochote kati ya sisi wawili, tumeshajadili na yameisha sasa mimi ni mtu huru.
Kuhusu mshindi wa Tusker Project Fame 2013, Msechu anasema: "Mshindi ni mshindi tu. Hope ni mzuri na ushindani ulikua mkubwa kwa hiyo yeyote ambae ameshinda ni mzuka."
Msechu amesema kinachofanya washindi wengi wa Tusker kutofanikiwa ni kulewa kutokana na zile pesa, inabidi wafundishwe jinsi ya kujiongoza kwenye maisha.
"Wenye njaa kama sisi ambao ndio tunakuwaga washindi wa pili ndio tunadunda mpaka leo."