
Kwa
mujibu wa Tino, wasichana warembo ni ‘chambo’ kinachowavuta wanunuzi wa
filamu za Tanzania. Ujuzi wa uigizaji na kipaji, si sababu kwao.
Akiongea
na gazeti la Mwanaspoti, Tino alisema warembo hao pamoja na kuzifanya
filamu zivutie pia huwa na juhudi katika kazi hiyo tofauti na wanaume na
wanaipenda kazi yao.
“Kwa
kweli bila kuweka wasichana warembo katika filamu yako hutauza kwa
sababu wengi wana juhudi za kufanya mambo mapya kila kukicha, lakini pia
wanakuongezea mvuto kwa kuwa warembo ni kama maua,”alisema Tino.
Pengine
ndio maana waigizaji wa kike wanaotamba ni walewale akina Wema Sepetu,
Lulu, Irene Uwoya, Jacky Wolper, Batulli na wengine waliojaaliwa sura za
kuvutia