
Ray C alisema japokuwa mama yake alitoa kwa umma mawasiliano yake na maelekezo ya namna ya kumsaidia, simu hiyo iliyokuwa busy saa 24, ilikuwa ikipokea simu na ujumbe kutoka kwa mashabiki wake pekee na sio msanii yeyote anayemfahamu.
Muimbaji huyo aliyewahi kutamba na vibao vingi vikali vikiwemo ‘Niwe
Nawe Milele’ Uko Wapi na Sogea Sogea, alisema hiyo ilimpa funzo kuwa mtu
maarufu huwa na marafiki pale tu anapokuwa juu lakini akipata matatizo
hutengwa na hata watu wake wa karibu.
Katika kipindi hicho pia, Ray C aligusia jinsi ambavyo Lord Eyez
alimuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ambapo alikuwa
akimchanganyia unga kwenye bangi bila ya yeye kufahamu na kwamba
alifanya hivyo kwa mwaka mzima.
Alisema baada ya kujigundua kuwa tayari ameingia kwenye tatizo kubwa
aliamua kuchukua uamuzi wa haraka wa kuachana na rapper huyo ingawa
anasema alikuwa akimpenda kwa dhati.
Katika hatua nyingine, Ray C alisema hakuna mtu anayeweza kumshukuru
zaidi kama Rais Jakaya Kikwete ambaye alimuelezea kuwa ni mtu mwenye
moyo wa kipekee kwakuwa amemsaidia kwa hali na mali na kumtoa kutoka
kwenye janga la uteja.
Aliongeza kuwa Rais Kikwete amekuwa akiwasaidia vijana wengi wenye matatizo hayo na sio yeye peke yake.
Alisema kwa sasa tayari amesharekodi nyimbo takriban 12 na
watayarishaji tofauti wa muziki akiwemo Tudd Thomas na Ema The Boy na
kwamba hivi karibuni ataachia wimbo wake mpya.
<< TIMES 100.5 FM>>
<< TIMES 100.5 FM>>