MWALIMU
Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo
za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku
akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za
kishirikina.
Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Tukio
hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma
Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa
anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar
es Salaam.
Akizungumzia
tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala
chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma
kutokana na kuwa na usingizi mzito.
Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Kwa
upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa
kufanya kazi kutokana na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.
Akizungumza
kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis
Milanzi alisema walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia
kuzihama nyumba zao kwa muda na badala yake kwenda kukesha kwenye
ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.
Ofisa
elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za
tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati
utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi
aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha mwalimu
huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo
kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Hili
ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la
kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa
shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule akiwa uchi wa mnyama
