Wanandoa mastaa, Beyonce Knowles na Jay Z wamekuwa wakihudhuria sherehe mbalimbali licha ya kuwepo uvumi kuwa ndoa yao ipo matatani lakini tetesi hii inaweza kuwa kubwa zaidi kuwahi kusemwa.
Kuna tetesi kuwa Beyonce amekuwa akimsaliti mumewe na kutembea na bodyguard wake Julius De Boer.
Beyonce anadaiwa kuwa karibu mno na Julius De Boer, mzaliwa wa Uholanzi ambaye amekuwa akimlinda tangu mwaka 2009. Habari zimedai kuwa Jay Z ana wasiwasi pia na uhusiano wao.
“Jay kiukweli anahisi kuwa kunaweza kuwa na kitu cha kimahaba kinaendelea kati ya Bey na Julius,” chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Mstarz News. “He wanted to fire Julius last February, but BeyoncĂ© said, ‘Julius isn’t going anywhere. They’ve spent a lot of time together behind closed doors. He’s even stayed in her hotel room.”
Kumekuwepo na tetesi za wawili hao kupeana talaka japo wamekuwa wakiikwepa. Tukio la Jay Z na Solanga kugombana kwenye lifti hivi karibuni liliongozea nguvu tetesi hizo.