
LAWAMA! Msanii maarufu katika tasnia ya filamu Bongo, Julieth Samson ‘Kemmy’ amesema wasambazaji wa filamu Bongo wamekuwa kikwazo cha mafanikio yao.
Msanii maarufu katika tasnia ya filamu Bongo, Julieth Samson ‘Kemmy’. Akipiga stori na paparazi wetu, Kemmy alisema wasambazaji ndiyo chanzo cha umaskini kwani wamekuwa
wakichelewesha filamu kuingia sokoni kwa kuziweka muda mrefu hata kufikia zaidi ya miaka miwili bila kuingia sokoni.
“Kwa mfano mimi nina filamu ina miaka miwili iko kwa wasambazaji na bado haijaingia sokoni huoni kama ni tatizo?’’ alihoji Kemmy.