
The big boss wa TMK Family Said Fella kwa sasa ameingia kwenye uvumi ulioenea kuwa yeye anachangia kuwadidimiza wasanii ambao wanakuwa na bifu naye ili wasiweze kusikika tena, hapa Fella anafunguka juu ya hutuma hizo.
”Sio kweli mimi siko hivyo kabisa na ninashangaa watu wanaosema kuwa nina wadidimiza wasanii niliokuwa na Bifu nao ili wasiweze kusikika tena kwenye game wakati sio kweli, mimi sina tabia hiyo kwa hiyo watu wasinifikilie hivyo kwani mimi ninapenda sana muziki wetu uzidi kukua na kufanya tuwe na wanamuziki wa kimataifa.” alisema Said Fella