Latest Updates

MUNGU SI ATHUMANI: HATIMAYE YULE MTOTO BONGE KUPELEKWA INDIA!

HATIMAYE Mtoto Grace Simon (14) (pichani) ambaye ameacha shule kutokana na tatizo la unene wa kupindukia, sasa atapelekwa India kwa ajili ya matibabu kwa gharama za serikali.
Mtoto Grace Simon (14) ambaye ameacha shule kutokana na tatizo la unene wa kupindukia. Mama mzazi wa Grace, Ashura Bakari alimwambia mwandishi wetu kuwa baada ya gazeti hili kuandika habari za mwanaye mara kwa mara, serikali imesikia kilio cha Grace ambaye ni mwanafunzi katika Shule ya Msingi Amani Ukonga, Ilala, jijini Dar es Salaam.

“Sehemu kubwa ya maagizo niliyopewa na wizara ya afya nimetekeleza ikiwa ni pamoja na kukamilisha viza na niliambiwa niende Jumanne (leo) kupata maelekezo zaidi,” alisema mama huyo.

Mama huyo alisema wasomaji wengi wa gazeti hili walimsaidia mtoto wake kwa hali na mali na amewashukuru kwa kuonesha huruma kwa mwanaye.

Mtoto Grace akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mmoja wa maofisa kutoka wizara ya afya ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, aliliambia gazeti hili kuwa tatizo kubwa la Grace ni homoni hazina uiano ndiyo maana zinasababisha moyo kujaa mafuta na uzito kuongezeka na kupungua kidogo bila utaratibu.

Afisa huyo alithibitisha serikali kumgharamia safari ya India mtoto huyo.

Mtoto huyo wakati anafanyiwa mahojiano na gazeti hili Januari mwaka huu, alikuwa na uzito wa kilo 111 hali iliyosababisha alazwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa wanaotaka kumpa pole mama wa mtoto huyo, Ashura Bakari wanaweza kuwasiliana naye kwa namba 0753 530 255 au 0719 465 443.