Latest Updates

HUSSEN MACHOZI AFUNGUKA SAKATA LA KUFUMANIWA NA MKE WA MWANASIASA MAARUFU NCHINI KENYA




MWANAMUZIKI aliyoibuliwa na wimbo wa ‘kwa ajili yako’ Hussein Machozi amefunguka na kuelezea tukio la kufumaniwa na mke wa mwanasiasa nchini Kenya na kudai kuwa jambo hilo halina ukweli wowote.

Katika mahojiano na kipindi cha Amplifire, alisema siku ambayo tukio hilo lilitokea alikuwa na mwanamke ambaye walikuwa wanapanga namna ya kufanya naye kazi katika moja ya hoteli nchini humo.

Lakini wakati wakiwa kwenye maongezi alikuja mwanaume mmoja ambaye anadai walikuwa na mahusiano na mwanamke huyo na kumfanyia fujo kutokana na ugomvi uliokuwa ukiendelea katika mahusiano yao.

Hata hivyo Machozi alisema alifanikiwa kutoka eneo hilo salama na kushangaa kwa nini jambo hilo limekuzwa sana.