Latest Updates

ISABELA NA KALAMA WAMWAGANA



Ule uchumba wa muda mrefu wa wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya, Isabela Mpanda an Kalama Bakari ‘Luteni’ umevunjika kwa kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa uaminifu baina yao.

Chanzo makini kilicho karibu na nyota hao wawili, kilisema kuachana kwao kunatokana na Luteni Kalama kukosa uaminifu kwa mwenzake kwani mara kadhaa, Isabela alizifuma meseji za wanawake wengine kwenye simu yake.

Kana kwamba haitoshi, Kalama ambaye ni memba wa Kundi la Gangwe Mobb, pia hivi karibuni, licha ya kutotokea kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Isabela, lakini alishindwa hata kumtumia ujumbe wa kumtakia heri.
“Ni kweli nimeamua kujiweka pembeni kwa sababu Kalama siyo mwaminifu, nilikuta meseji mbalimbali za mapenzi za wanawake wengine, naogopa Ukimwi, bora nikae pembeni nimuache aendelee kufanya umalaya wake maana huyu ni sikio la kufa,” alisema Isabela baada ya kutakiwa kutoa ufafanuzi wa habari hizo.
“Kilichoniumiza zaidi, hivi karibuni ilikuwa bethidei yangu hata hajani-wish kunijulia hali wakati nilikuwa ninaumwa, bora niendelee na maisha yangu, ndiyo maana mmeona hata kwenye uzinduzi wa Global Tv kila mtu alikuja kivyake.”
Kalama alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Mimi sijui kama tumeachana, lakini kama Isabela ameamua hivyo ni sawa tu, ninachojua kila mtu yupo kwake, mimi niko Tabata yeye Kijitonyama.”