Latest Updates

JAJI WARIOBA AFUNGUKA, ASIKITISHWA NA KAULI ZA VIONGOZI CCM



Hatimaye Jaji Warioba amefunga na kusikitishwa na upotoshaji mkubwa sana unaendeshwa na viongozi wa CCM juu ya Rasimu ya katiba. Amesema kuna uongo unaokuzwa kuwa Serikali tatu inasababisha jeshi kuchukua nchi, amesema kwanini iwe jeshi tu na wasiwe walimu nk? Akaendelea kusema kuwa akiwa Waziri mkuu mara zote alipokuwa akifanya ziara mikoani alikuwa akitembelea maeneno yenye kambi za jeshi, anasema kulikuwa na hali ngumu sana lakini bado wanajeshi wale waliendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa. Anajiuliza Je, kwanini awakupindua nchi wakati huo. Amesema kinachosikitishwa ni kauli hizi kutolewa ndani ya makanisa na sehemu za ibada, jambo ambalo amesema kuwa linaweza kuwa ni kuwagawa watanzania kwa itikadi za dini nk. Jaji Warioba akiwa na uso unaonyesha huzuni amesema kuwa wanasiasa na hasa wa chama tawala wanaweza wakalipasua Taifa na kuleta madhara makubwa kwa Taifa mbeleni.

Source: EATV hot mix