Latest Updates

Club 40/40 Nyingine Ya Jay Z Kufunguliwa Kwenye Kiwanja Cha Ndege.


Mtandao wa burudani The Source umeripoti kuwa Rapper Jay Z amefikia makubaliano ya kufungua Club ya 40/40 kwenye Kiwanja cha ndege kikubwa Marekani kilichopo miongoni mwa viwanja vinavyo pokea na kusafirisha abiria wengi zaidi duniani. Mpaka sasa eneo linalohusika na michezo kwenye club ya 40/40 limeshafunguliwa ila bado club yote haijakamilika.

Club hii ipo kwenye eneo la Kiwanja cha kimataifa cha Ndege Hartsfield-Jackson kilichopo mjini Atlanta

Msemaji wa kiwanja hicho cha ndege amesema kuna mpango wa kuwepo na eneo la VIP kwenye club hio ambalo litakuwa tofauti na sehemu ya michezo.

Fahamu Rapper Jay Z alifungua 40/40 Club ya kwanza mjini Manhattan akishirikiana na mfanya biashara mwenzake Juan Perez mwaka 2003. Club ya 40/40 pia ipo Barclays Center mitaa ya Brooklyn.

Mpaka sasa Imefikia Hapa.

Jay Z alisema mapema kuwa muonekano wa club hii utakuwa tofauti na hii hapa chini ambayo ni club 40/40 ya New York