Msanii aliyebahatika kuwa maarufu wa vichekesho Bongo, Silvery Mjuni ‘Mpoki’ au Bepari la Kihaya.
Hata hivyo, ikiwa msanii huyo ambaye kwa fikra zake anaamini ndiye
mkali kuliko wachekeshaji wote Bongo japokuwa Mzee Majuto ndiye namba
moja, anaweza kuwa mwerevu badala ya kuendelea kuwa mjinga.
KWA NINI MJINGA?
Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Oxford – Toleo la Pili) inamuelezea mjinga kuwa ni mtu asiyejua kitu au jambo fulani.
Hata hivyo, mjinga hawezi kuendelea kubaki katika hali hiyo baada ya kufundishwa na kujua maana.

HABARI KAMILI
Tukio la Mpoki hivi karibuni kuwadhalilisha watu waliofika jukwaani kukabidhi tuzo kwa washindi katika Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ni ushahidi tosha kuwa ana tatizo la kufikiri.

Ukiachana na tukio hilo, rekodi yake ya maisha yake ya kisanii na nje
ya sanaa inathibitisha asivyo hodari wa kutumia ubongo wake sawasawa,
vijana wa mtaani huita zero brain (0).
Kwa uelewa wake, uchekeshaji ni udhalilishaji ndiyo maana vipande vingi anavyoigiza huwa anawasema watu vibaya hata wale ambao wamemsadia kufika alipo kisanii.
Kwa uelewa wake, uchekeshaji ni udhalilishaji ndiyo maana vipande vingi anavyoigiza huwa anawasema watu vibaya hata wale ambao wamemsadia kufika alipo kisanii.
TUZO ZA KILI
Katika hali ya kawaida, kwa mtu asiye mjinga na anayejitambua, Mpoki asingeweza kumkejeli mtu mwenye heshima zake kama Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa Aset.
Katika hali ya kawaida, kwa mtu asiye mjinga na anayejitambua, Mpoki asingeweza kumkejeli mtu mwenye heshima zake kama Asha Baraka ambaye ni Mkurugenzi wa Aset.
Asha anaweza kuwa mama yake lakini bila haya alimwambia mbele ya
hadhara kuwa kwa alivyo na mwonekano mzuri kwa usiku ule, asubuhi yake
angeweza kusalimiwa shikamoo (akimaanisha angekuwa na mwonekano wa kizee
kwa kuwa hatakuwa na make up tena).
Hakuishia hapo, Mpoki alifikia hatua ya kuingilia hadi mambo binafsi
ya watu ambayo katika hali ya kawaida hayawezi kuwa utani, alimwambia
Maimartha Jesse kuwa licha ya kwamba ananyonyesha lakini amepiga matiti
jeki. Upuuzi mtupu!
NJE YA KILI
Ukiachana na kero alizotoa kwenye jukwaa lile linaloheshimika, Mpoki ana tabia ya kuwadhalilisha watu hata anapokuwa kwenye kazi zake. Mifano ipo mingi.
Ukiachana na kero alizotoa kwenye jukwaa lile linaloheshimika, Mpoki ana tabia ya kuwadhalilisha watu hata anapokuwa kwenye kazi zake. Mifano ipo mingi.
Kutokana na kile kinachoonekana kutojielewa, Mpoki humkejeli mtu
makusudi ili kutengeneza bifu akiamini magazeti yakimwandika ataendelea
kuwa juu.
Hivi karibuni alitoa wimbo ambao ndani yake amewatukana baadhi ya
watu akiwemo mwandishi mmoja mashuhuri nchini wa magazeti pendwa kwa
kumuita dada wakati akijua ni mwanaume (anapenda misala).
Kwa akili zake fupi, aliamini paparazi huyo angepaniki na kurushiana
naye maneno kwenye magazeti na mitandao ya kijamii, hakufanya hivyo na
mpaka sasa yuko kimya kabisa kama hakuna kitu kilichotokea kwa sababu ni
mwerevu.
Pia jamaa huyo bila haya wala soni aliwahi kuigiza kwa kumkejeli
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi kwenye maigizo yao ya
Orijino Komedi.
Ikumbukwe kuwa, Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) inayomilikiwa
na mzee Mengi ndiyo iliyorusha kipindi chao cha vichekesho kwa mara ya
kwanza. Kifupi ndiye aliyemtoa baada ya kupigika kwa muda mrefu.
Mpoki alitambulishwa kwa mara ya kwanza na Runinga ya ITV akiwa na
Kundi la Nyota Ensemble kupigtia Kipindi cha Mambo Hayo cha ITV ambacho
ni mali ya mzee Mengi.
WADAU WACHARUKA
Wadau wa burudani Bongo waliopata kuzungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, walionesha hisia zao za wazi kwa namna walivyokasirishwa na msanii huyo mwenye mdomo mchafu na asiyepima maneno.
Wapo waliokwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba ikiwa kutakuwa na shughuli yoyote ya kiburudani na msanii huyo akapangwa kuwa MC basi hawatahudhuria kwa kuogopa kudhalilishwa.

Nasra Abdillah wa Tabata jijini Dar alisema: “Mimi nahisi kuna kitu
cha zaidi kwa Mpoki, si kwamba ni mchekeshaji, nadhani kichwani hayupo
vizuri. Mimi nilikwenda Mlimani City siku ile, kuna ndugu yangu alikuwa
mmoja wa watoa tuzo.
“Alipoona kila anayepanda anadhalilishwa (ingawa kwa Mpoki ni utani)
akaingiwa hofu. Ilifika mahali akatamani kuahirisha kwenda kutoa tuzo,
tukampa moyo lakini alipopanda mambo yakawa yaleyale, akadhalilishwa
waziwazi.
“Mpoki anatakiwa kubadilika. Nampa ushauri wa bure, ajifunze kupitia
kwa wengine. Lakini hata hivyo mimi popote ambapo yeye atakuwa
mshereheshaji, sitakanyaga hata kwa dawa.”
Dulla wa Sinza Kwaremmy alisema: “Sikufurahishwa na kitendo cha
kumwambia Dj Bon Love na wadogo zake kwamba ni wabahili wa fedha na
kumshangaa Vanessa Mdee kwa kuzungumza Kiingereza wakati yeye ni Mpare
azungumze Kiswahili, halafu akamkejeli eti awe anafanya mazoezi ya kuvaa
viatu virefu baada ya kunusurika kuanguka jukwaani. Ule si utani ni
udhalilishaji.”
Mdau mwingine ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema:
“Sikufurahishwa kabisa alivyomwambia Isha Mashauzi, eti ni mwanamke wa
Kikurya, si wa kuoa.