Latest Updates

JESHI LA POLISI LINAMSAKA ASKARI WAKE ANAYEJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA MENO YA TEMBO


Jeshi la polisi mkoani Lindi linamtafuta askari wake mmoja mwenye namba F6508 Detective Constable JOSEPH YONA MASANJA mwenye Umri wa miaka 34 mzaliwa wa Wilaya ya ILEMELA Mkoani MWANZA Abae alikuwa akifanya kazi kituo cha polisi KILWA kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa vipande 62 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 568 yaliyokuwepokituoni hapo kama Vielelezo.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi,Kamishna Msaidizi Renatha Mzinga alipokuwa Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kufuatia jitihada mbalimbali za kumtafuta kutoleta Mafanikio.

Mtuhumiwa Huyo ambae alikuwa mtunza Vielelezo katika kituo cha polisi Wilayani Kilwa toka mwaka 2004 ambaye kwa sasa amefukuzwa kazi kutokana na utoro kazini ,kabla ya kugundulika kwa wizi huo baada yakuomba ruhusa ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha DSM ambako baada ya uchunguzi alibainika kuwa alibadili chuo na kwenda chuo kikuu cha SAUT -Mwanza ambako hata hivyo amebainika ametoweka.

Kufuatia kutoweka kwake Jeshi la polisi mkoani LINDI limewaomba wananchi kutoa taarifa za mtuhumiwa huyo popote watakapomuona kwani ametumia nafasi yake vibaya na kuhujumu rasilimali za taifa kwmanufaa yake binafsi.

'ndg zangu wanahabari naomba mtusaidie maana Huyu jamaa Mara ya mwish alikuwa Chuo cha SAUT cha Mwanza tulipomfuatialia akawa ametoweka ghafla na suala tulilibaini baada ya vielelezo hivyo kukataliwamahakamani na maafisa wanyamapori kuwa si vyenyewe na vina upungufu mkubwa ikiwemo kupunguzwa ukubwa wake.

Katika tukio lingine Kamanda Mzinga alieleza kuwa polisi wamemkamata SAID ALLY MASOUD katika kisiwa cha POMBWE wilaya ya KILWA akiwa amejeruhiwa vibaya na bomu alipokuwa akivua samaki kinyume cha sheria kwa kutumia baruti.

Mtuhumiwa huyo amelazwa katika hospitali ya KILWA ya KINYONGA na hali yake imeelezwa kuwa ni mabaya kiasi cha kushindwa kujieleza baada ya baruti kumfyatukia yeye badala ya samaki.