Home » Uncategories » MASIKINI..!! JAMAA AJINYONGA BAADA YA MKE KUMWAMBIA AMELEA MIMBA YA WATOTO MAPACHA WA MWANAUME MWENZAKE
MASIKINI..!! JAMAA AJINYONGA BAADA YA MKE KUMWAMBIA AMELEA MIMBA YA WATOTO MAPACHA WA MWANAUME MWENZAKE
Na Marco Mipawa, Geita
Mkazi wa mtaa wa Tambuka reli mjini Geita Antony Komba (30) amefariki dunia kwa kujinyonga usiku wa kuamkia leo kutokana na kile kinachohisiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Imeelelezwa kwamba jana jioni Marehemu Komba alikuwa na ugomvi na mke wake Vumilia Msomi(29) nyumbani kwao, baada ya mke wake kumtamkia kwamba watoto watatu wa miezi tisa wanaowalea, mwanamke huyo amezaa na mme mwingine.
Kamanda wa polisi mkoani Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi Joseph Konyo amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba Marehemu Komba alikuwa ameandika historia ya maisha yake tangu alipomuoa Msomi.
Konyo amesema katika historia hiyo Komba ameeleza jinsi alivyohangaika kulea mimba ya watototo hao Mapacha akiwa na mama yake mzazi anayeishi mkoani Tabora hadi kufikia jana alipoambiwa kwamba watoto hao hawakuwa wa kwake.
Shemeji wa marehemu Komba Pendo Msomi aliyekuwepo kwenye tukio amesema, Komba baada ya ugonvi na mkewe alienda kulala, na ilipofika saa 2:00 usiku aliondoka nyumbani kwa madai kwamba anakwenda kuangalia mpira na hakurudi nyumbani.
Mwili wa marehemu Komba umeokotwa ukiwa umening’inia kwenye mti wa Mpera na jeshi la Polisi wilayani humo linaendelea na kumtafuta Msomi aliyetoroka na kutokomea kusikojulikana mara baada ya kugundua kuwa amesababisha kifo cha mme wake.
Posted