Nahodha wa Meli ya Korea Kusini Afunguliwa Kesi ya Mauaji
Nahodha wa Meli ya Korea Kusini iliyozama mwezi uliopita ikiwa na wanafunzi wengi, amefunguliwa mashitaka ya mauaji pamoja na wenzake watatu.
Kwa mujibu wa CNN Muendesha mashitaka mkuu, Yang Joon-jin amemtaja nahodha huyo kwa jina la Lee Joon-seok, fundi mitambo na wafakazi wengine wawili wa karibu katika ngazi za juu za meli hiyo kuwa wanaweza kukabiliwa na hukumu ya kifo endapo watakutwa na hatia.
Hata hivyo, ni miongo miwili tangu adhabu ya kifo itekelezwe katika nchi ya Korea Kusini.
Wafanyakazi wengine 11 wao wanakabiliwa na mashitaka ya kuwatelekeza abiria bila kuwapa msaada wa kutosha wakati wa ajali hiyo kitendo ambacho ni kinyume cha sharia ya usalama katika safari za meli.
Posted