Taarifa kuhusu kutangazwa kwa kocha mpya wa Man Utd
Wiki kadhaa baada ya kumtimua kocha David Moyes klabu ya Manchester united wanakaribia kumtangaza kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van Gaal kuwa meneja mpya wa timu hiyo.
Mholanzi huyo tayari ameshakubali kuchukua madaraka ya ukocha Old Trafford lakini bado ana kazi ya kuiongoza Uholanzi kwenye michuano ya kombe la dunia na maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo yamesababisha dili lake na United kuchelewa kukamilika.
Mwanzoni iliripotiwa kwamba angetambulishwa mwishoni mwa wiki hii lakini badala yake ameendelea kubaki nchini Uholanzi na inaaminika sasa atatambulishwa wiki ijayo baada ya mchezo wa kirafiki.
Jana Ryan Giggs ambae ameshika madaraka ya ukocha kwa muda alisafiri mpaka Uholanzi ambapo alikutana na Van Gaal mjini Noordwijk kwa ajili ya kuzungumza juu ya Giggs kupewa madaraka ya kocha msaidizi pamoja na mipango ya usajili msimu ujao.
Posted