Mwigizaji wa filamu Bongo, Kajala Masanja ‘Kay’.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza-Madukani jijini Dar.
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.

Pichani ni mjengo ambao Kajala Masanja amepanga.
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.

WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.

Gari la aina ya Toyota Brevis inayomilikiwa na Kajala.
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa
likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu
ambalo ni Toyota Harrier.
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina gazetini, rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.

Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu akitafakari jambo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
“Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume, jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaoni