MWANADADA anayefanya poa kwenye anga la filamu
Bongo, Lucy Komba amejikuta akibaki na viulizo vingi kutokana na kitendo
cha msanii mwenzake, Aunt Ezekiel kuishi mbali na mumewe anayefahamika
kwa jina la Demonte kwa kipindi kirefu, jambo ambalo yeye hawezi
kulifanya.
Mwanadada anayefanya poa kwenye anga la filamu Bongo, Lucy Komba.
Akizungumza na paparazi wetu, msanii huyo alisema kitendo cha Aunt
kuolewa na kuishi mbali na mumewe kinamfanya abaki na maswali mengi
kichwani, sababu wanandoa kuishi mbalimbali husababisha wahusika
kuumizana kichwa kwa kiasi kikubwa na kukosa amani ya moyo.
Aunt Ezekiel
“Namshangaa Aunt anawezaje kuishi mbali na mumewe kwa kipindi kirefu,
binafsi siwezi. Kama hivi ninavyotarajia kuolewa hivi karibuni,
nimekubali kuachana na dili zangu zote za hapa Bongo, nikiolewa naenda
kuishi Denmark kwa mume wangu,” alisema Lucy Komba.