Latest Updates

LINAH ANENA MANENO MAZITO KUHUSU WASANII WENZAKE HASWA WA KIKE

Katika historia ya muziki wa kizazi kipya nchini ni nadra kwa wasanii wa kike kushirikiana katika kazi zao, ikilinganishwa na wenzao wa kiume.

Yalikuwapo makundi kadhaa likuwamo Kankaraga (Quenns of Swagger), Scopion Girls lililoundwa na Jack Pentezel, Miriam Jolwa (jini kabula) na Isabela Mpanda (Bela), The Trio lililoundwa na Kadja Nito, Angel Karashani na Alice.
Hata hivyo, makundi hayo yamekuwa yakitofautiana na mwishowe baadhi yalivunjika.
Historia inaonyesha kuwa imekuwa ni nadra kwa wasanii wa kike nchini kufanya kazi pamoja huku mwimbaji Estelina Sanga maarufu Linah akiibeba historia hiyo kutokana na kukubali kushirikishwa na msanii chipukizi Kadja Nito katika wimbo wa ‘Mke Mwenzangu’.
Katika mahojiano yafuatayo pamoja na mambo mengine, Linah anazungumzia kasumba iliyopo kwa wasanii wa kike nchini kutopendana, akiweka wazi kwamba kwake milango ipo wazi kwa yeyote anayetaka kushirikiana naye, ikiwa anajituma, akiwa pia na kipaji.
“Masuala ya kushikana mkono huku umebweteka sitaweza. Mtu atakayekuja kwangu, aniambie nimetafuta huku, nimehangaika nimefika hapa na wimbo wangu huu nifanyeje? Siwezi kumkatisha tamaa huyu ni lazima umtie moyo,”anasema.
Linah anaweka wazi kuwa yeye pia alisaidiwa na watu aliowakuta katika fani hiyo, akieleza: “Nimeingia THT nimemkuta Recho, nimefika pale mwaka mmoja tu nikatoka, yeye alikuwa na miaka mitatu pale na hajatoka bado, lakini alijitahidi na baadaye akafanikiwa.”
Anasema tatizo kubwa ni masengenyo na vikwazo vinavyowafanya wengi washindwe kukubali kufanya kolabo na wasanii wenzao.
Anabainisha kuwa hayo yalishawahi kumtokea yeye pia.
“Sisi wasichana tuna wivu sana, kuna wasanii wawili niliwafuata lakini wakaanza maneno pembeni, ndiyo maana wasichana tupo wachache kuliko wanaume katika fani hii. Nilipoenda Afrika Kusini na kufanya kazi zangu, sasa wameanza maneno, nimeyasikia jambo ambalo siyo kweli. Wanasema ooh, ana mabwana wamempeleka kule na kumuunganisha.Jamani mtaishia hivyo hivyo ni kujituma tu ndiyo silaha.”
Hata hivyo, Linah anasema: “Mambo kama haya yanaturudisha nyuma, hebu tuangalie wenzetu Rihanna na Shakira, wamefanikiwa katika kazi zao, ukiangalia kwa hapa nchini hakuna kolabo zaidi ya mimi na Khadija, sisi ni wa kwanza kwa wasichana.”
Anasema hilo lilijidhihirisha wakati ilifanyika kolabo ya Prokoto kati ya Ommy Dimpoz, Diamond na Victoria Kimani.
Linah anasema badala ya kutafuta uhusiano, wasanii wengi wa kike hapa nchini waliingia kwenye kusengenya.
“Wakati Victoria Kimani amekuja, sikuwa hapa nchini nilikuwa Afrika Kusini, kwanza nakumbuka nilimpigia simu Diamond nilimwambia ningekuwapo ningefanya naye kolabo, unajua mimi ni mtu wa kujipendekeza sana,” anasema Linah.
Akizungumzia muziki wake kwa sasa, Linah anayefanya kazi chini ya lebo ya; No Fake Zone ya Afrika Kusini, anasema kuwa amefanikiwa kuifikia ndoto aliyokuwa nayo maishani mwake kutokana na kujipanga.
“Nikisema najipanga huwa najipanga kweli, ndoto yangu ilikuwa ni kuja kuwa mwanamuziki wa kimataifa, nilijipanga na nashukuru Mungu kwamba nimefanikiwa.
Nilisafiri nikajifunza vitu vingi, nashukuru Mungu nimeweza kufikia lengo,” anasema Linah anayetamba na wimbo ‘Ole Themba’.
Linah anasema : “Kufanya kazi na watu wengine nimejifunza mengi siyo kitu cha mchezo. Aina Uhuru, Eskido na wengineo ni wasanii wakubwa sana, wenzetu wameendelea kutokana na mafunzo waliyopewa, kitu kikubwa zaidi nimejifunza ni kuingiza sauti.”
Msanii huyo nyota anasema kuwa katika tasnia hiyo ni kama mtu anavyoamka asubuhi kwenda kazini na msanii unapaswa kujiweka vizuri na kujithamini mwenyewe kwanza.
“Nakumbuka nilivyokuwa nikifanya kazi na God Father, aliniambia kwamba ni muhimu msanii kuhakikisha hashuki chini, anatakiwa aendelee na mwendo huo, alinishauri sana,”anasema.
Maisha
Kuhusu maisha na kazi Linah anasema: “Cha kwanza ukiwa msanii unatakiwa kujitambua, lakini pia kutambua shabiki ni mtu anayeweza kukugeuka. Mtu wa nje hatakiwi kujua kitu gani umefanya ili uwe vile ulivyo.”
Anaongeza: “Inawezekana kutengeneza fedha nyingi kupitia muziki wa Tanzania, unapanga mwenyewe, lakini wengi wetu tunapenda zaidi starehe. Baadhi ya shoo zilinisaidia kuhifadhi fedha kwenye kibubu.
Fedha za shoo zimenisaidia kufanya mambo mengi, wengi wanajisahau kwamba wanatakiwa kupanga kipato chao. Wengi tunajisahau, mwisho wa siku Linah nikifanya hivi, yanaanza maneno ya uzushi, aah kahongwa yule, jambo ambalo siyo zuri.”
Linah anaeleza kuwa msanii ni mtu wa kwanza kujitengenezea mazingira ya kuheshimika na kupendwa.
“Tujitengenezee mazingira yatakayotupandisha. Kuna wakati tunakata tamaa, msanii fulani anafanya muziki kama wangu, tusibweteke tupambane, muziki ni