Latest Updates

MARIO BALOTELI ATEMWA NA KIKOSI CHA ITALIA

































Mshambuliaji wa Liverpool Mario Baloteli ameachwa kwenye kikosi kipya cha kwanza cha Italia na kocha Antonio Conte.
Mchezaji huyo mwenye miaka 24 angeweza kucheza mechi ya kirafiki na Uholanzi Alhamis ya wiki hii, lakini amefungiwa kucheza mechi za kufuzu za kushiriki kombe la Ulaya huko Norway.
Balotelli ambaye amesainiwa kwa ada ya uhamisho pauni milioni 16, amesimamishwa kucheza baada ya kupata kadi mbili za njano katika kombe la dunia.
Kocha huyo wa zamani wa Juventus Conte, ameichukua nafasi ya Baliotelli na kumpa Cesare Prandelli, ambaye alijitoa kwenye timu yake baada ya Italia kutolewa katika hatua ya makundi kwenye kombe la dunia.
Naye kiungo wa Sunderland Emanuele Giaccherini amekuwa ni mchezaji pekee mwenye asili ya Uingereza katika kikosi hicho cha wachezaji 27.