AINA HII YA WANAWAKE NDO HUWADATISHA ASILIMIA KUBWA YA WANAWAKE
WENYE MSIMAMOWanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni
wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, walio
makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata
mafanikio.WAPENDA USAWAAina ya pili inayohitajika katika ulimwengu wa
kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba
majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa
kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.WANAOJUA MAPENZIWanawake wajuzi wa
mamboya faragha wanapendwa sana. Sifa yao kubwa ni uwezo wa
kuwatosheleza wenzi wao katika tendo la ndoa. Tafiti zinaonesha
kuwawanaume hupenda sana wanawake watundu katika mchezo wa sita kwa
sita. Mara nyingi wanatajwa kuwa na uwezo wa kuteka akili za wanaume
bila kujali sifa zao za nje au za
ndani.MARAFIKIWanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne
inayowavutia wanaume. Waohutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana
na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa
kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, ni waungwana na
wapenda amani.WAPENDA UWAZIAina nyingine ya wanawake inayowavutia
wanaume ni wenye msimamo na wapenda uwazi. Si wepesi wa kuburuzwa katika
maamuzi ya msingi kwa kisingizio cha wao ni wanawake. Utafiti
unaoneshawanawake wa aina hii wamekuwa muhimu hasa kwa wanaume wenye
tabia za ubabe na udhaifu katika uelewa wa mambo.WANAOJITEGEMEAWanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume
tofauti na akina ‘naomba vocha’ kila siku. Uchunguzi unaonesha kuwa
wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na
wanaoendekeza starehe za upande mmoja.WASIO NA PRESHANikisema wanawake
wasiokuwa na presha namaanisha wasiolazimisha vitu vitokee haraka
haraka. Wao siku zote huacha mambo yatokee yenyewe na kazi yao kuwa ni
kutenda sehemu ya majukumu yao kama wapenzi.MARIDADIKundi lingine la
wanawake wanaopendwa nawanaume ni wanaozingatia usafi na kujiremba.
Wanaokwenda na wakati katika mavazi na mvuto wa nje lakini pia ni
waelewa wa mazingira, si washamba. Wanapendeza kwa
mwonekano.WANAORIDHIKAWanawake ambao huridhika na hali walizonazo ni
kivutio kikubwa kwa wanaume. Hili ni kundi linalohitajika sana katika
ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa
yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote
bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.WA MMOJAWanawake
wanaochagua mara moja na kutosheka na kuwa tayari kukwepa kila aina ya
vishawishi toka kwa wanaume ambao kimtazamo wana vitu vya ziada zaidi ya
waliowachagua mwanzo, wanahitajika sana. “Niliye naye ananitosheleza
kwa kilakitu sitaki mtu mwingine.” Kundi la wanawake wa aina hii ni
adimu na muhimu sana.
Posted