Latest Updates

USIMWITE KAJALA BALI NI MADAM KAJALA

kajala
Msanii wa filamu na mmiliki wa Kajala Entertainmenrt, Kajala Masanja, mpaka sasa ameshafanya filamu zaidi ya mbili katika kampuni yake na anasubiri aanze kuziachia kwa wakati yeye na management yake. Kajala ambaye alikuwa rafiki mkubwa sana wa Wema Sepetu ila baadae walikuja kutofautiana, kwa sasa Kajala ndiyo ameshika usukani kutokana kila event kutokea na Wema Sepetu atii miguu, swali kwanini Wema Sepetu atimbi kiwanja Kajala anachokuepo, kupitia mdakuzi wetu alitupasha hivi.

”Kwa sasa pesa kwa Kajala si tatizo kabisaa coz kwa siku anatumia zaidi ya milioni mbili kwake, akitembea anatembea na timu ambayo inambebea mikoba na kuangalia usalama wake yaani amekuwa kama Wema na yeye anaitwa Madam, kwa mfano kwa nyakati tofauti tofauti siku hizi akienda kwenye event huwa anatunza kwa kiwango cha laki nane hii inaonyesha yupo vizuri sana mfukoni, kwenye birthday ya Odama na juzi kwenye uzinduzi wa filamu ya ‘Mateso Yangu Ughaibuni’ nayo ilikuwa hivyo hivyo so yaani ni tajiri mtoto kwa sasa. Kutokana na hiyo ndiyo maana atakapokuwepo Kajala basi Wema hawezi kuwepo kiukweli kabisa haiwezi kuwa kama mwanzo katika urafiki wao. ” Kilisema chanzo chetu