Latest Updates

Mke awakurupusha mume na dada yake pacha waliokuwa wakichepuka ndani ya gari na kuwaacha uchi mtaani





Mwanamke mmoja nchini China, Ting Su, 29, alimshuku mumewe kuwa alikuwa akichepuka na dada yake pacha. Aliweka kisirisiri app inayoonyesha simu ilipo (phone tracker) kwenye simu ya mumewe.

Alipowashuku kuwa wapo pamoja, alifuata alipo mumewe Cheng, 30, na kumbamba akiwa anafanya ngono na pacha wake ndani ya gari. Aliwafurusha na wote wakaruka nje ya gari wakiwa uchi wa mnyama.

Walipotoka nje wakiwa uchi, Ting aliamua kutumia fursa hiyo kuwatia adabu. Ting aliingia kwenye gari na kuondoka nalo, akiwaacha wazinzi hao wakiwa bila nguo mtaani, huku mume akilikimbiza gari kumuomba afungue mlango walau wapate nguo zao.

Mmoja wa mashuhuda, You Meng, 33, alisema: ‘It was so funny. Loads of people were grabbing their phones and I did as well. He was banging his fist on the window and shouting at her, and she just wasn’t playing ball.’

Ting ameamua kudai talaka kutoka kwa mumewe Cheng kutokana na usaliti huo. Hatima ya uhusiano wake na dada pacha wake aliyemsaliti kwa kuchepuka na mumewe bado haijajulikana.



Mwanamke anaonekana akiwa ameshikwa na aibu baada ya kubambwa akifanya ngono na mume wa pacha wake



Mume akimuomba mkewe afungue mlango, wakati mke huyo akiondoa gari



Mume akiendelea kumbembeleza mkewe afungue mlango, lakini mama huyo aliamua kumwaga ugali baada ya dada yake na mume wake kumwaga mboga