Latest Updates

UNARINGIA UZURI NA SHEPU YAKO, VIPI HII LA FARAGHA?




Ulimwengu wa sasa umejaa wanawake wazuri sana, kila unayemuangalia unaona kuna vitu f’lani Mungu kamjaalia. Unaweza kukutana na msichana ambaye hana shepu kabisa lakini sura yake peke yake inamfanya awe tishio kwa wanaume.

Wapo pia wanawake ambao hawana sura ya mvuto lakini Mungu kawajaalia kuwa na maumbile tata yanayowatoa udenda wanaume wengi.
Kimsingi kila mwanamke ni mzuri.

Unaweza kukutana na msichana ukaona hana sifa za kuwa wako lakini kwa mwingine ikawa tofauti.
Ndiyo maana hakuna mwanamke anayefikia hatua ya kuwa na mpenzi na akakosa, kila mtu ana sifa za kupendwa.

Lakini sasa leo nataka nizungumzie wanawake ambao wako kwenye ndoa lakini ni mambumbumbu wawapo faragha. Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, kuna wanawake wazuri kwa kila kitu lakini wamekuwa wakishindwa kudumu katika ndoa zao.
Wengine ni wazuri lakini wanaishia kuchezewa na kuachwa, yani hakuna mwanaume anayetokea kutangaza ndoa.

Unadhani ni kwa nini? Swali hilo tutalipatia jibu hapa.
Lakini pia wapo wanawake wazuri sana ambao ukiwaangalia unaweza kusema Mungu kawapendelea, yaani ni wazuri wa kila kitu, kuanzia tabia, sura mpaka shepu.

Cha ajabu sasa wanawake hawa unaweza kukuta wanaongoza kwa kusalitiwa na waume zao.
Unadhani ni kwa nini? Jibu pia utalipata hapahapa leo. Kikubwa ambacho nataka kukieleza ni kwamba, wapo wanawake ambao wanajisifu kwa uzuri lakini wanajisahau katika sehemu moja ya msingi sana,

FARAGHA!
Huenda bado nimekuacha kwa kusema hivyo lakini unachotakiwa kunielewa ni kwamba, wapo wanawake ambao wamekosa mbinu sahihi za kuwashika waume zao na wapenzi hasa katika eneo la faragha.

Wao wamebaki kujisifia kwamba ni wazuri lakini wanashindwa kujiweka vizuri kwenye eneo hilo muhimu. Kwa wale wasiojua ni kwamba, mapenzi ni kama sanaa. Mwanamke anatakiwa kuwa mbunifu na mtundu wa hali ya juu ili kuhakikisha anamfanya mume au mpenzi wake ahisi amepata mtu sahihi.

Itakuwa ni jambo la ajabu sana kama utakuwa ni mwanamke lakini uwapo faragha na mtu wako unakuwa mshamba wa kutupwa. Yaani unakuwa hujui chochote. Unadhani katika mazingira hayo utaweza kumzuia mwenza wako asishawishike kutoka nje?

Ninaposema hivyo nisieleweke vibaya kwa kuwa najua kuna wale ambao wamekuwa mbali kabisa na mapenzi, yaani walikuwa hawajihusishi kwa namna yoyote na mambo ya mapenzi mpaka pale walipokuja kuolewa.

Hao wamefanya jambo jema ambalo linamfurahisha Mungu lakini sasa umeingia kwenye ndoa, umeweka jitihada gani za kuhakikisha na wewe unakuwa mtaalam kwenye mambo yetu yaleee?Unadhani utakuwa sahihi kusema mumeo hawezi kukusaliti wakati wewe mwenyewe ni mbumbumbu wa kutupwa linapokuja suala la mahaba? Mimi sidhani kama utakuwa sahihi.

Kitu muhimu kwa mwanamke ni kuhakikisha unakuwa mtundu na mbunifu wa mambo ambayo ukimfanyia mumeo, utamzubaisha na asishawishike kutoka nje.Ni kweli wanaume wanatakiwa kuwavumilia wake na wapenzi wao lakini wanawake nao wasikubali kupitwa na wakati.

Wajue kwamba ulimwengu wa sasa una changamoto nyingi za kimapenzi. Usaliti umekuwa ni mwingi kiasi kwamba kila mmoja anatakiwa kujiaminisha kwenye kumridhisha mwenza wake kwa kila nyanja.
Tusiwe watu wa kuyaacha mambo yajiendee tu, tunapokuwa tumeingia kwenye ndoa au kuwa na wapenzi tunakuwa ni watu wazima wenye akili. Basi tutumie akili zetu, maarifa na ujanja wetu kujipa elimu ya kutosha juu ya mapenzi.

Hilo litakufanya ujiamini na wala usiwe na hofu ya kusalitiwa.
Tunajua wapo wanaosaliti kwa hulka zao tu, yaani hata wafanyiwe nini kutulia ni vigumu. Hao wala wasituumize vichwa!