Latest Updates

Diamond kuungana na Mafikizolo kurekodi wimbo uitwao Tell Every One wa kampeni ya ‘The Global Goals’




Fresh kutoka kurekodi wimbo na Ne-Yo, Diamond Platnumz amekwea pipa kutoka Nairobi kwenda nchini Afrika Kusini kuungana na Mafikizolo kurekodi wimbo uitwao ‘Tell Every One’ ambao ni sehemu ya kampeni ya dunia ya kutokomeza umaskini, maradhi, njaa na matatizo mengine, The Global Goals.


Diamond na meneja wake Sallam wakiwa kwenye ndege kuelekea Afrika Kusini Ijumaa hii

Mafikizolo tayari wameshaingiza sauti zao na sasa anayesubiriwa ni Diamond ambaye huenda leo akamaliza sehemu yake.



Mchezaji wa Real Madrid, Gareth Bale naye ni sehemu ya mastaa duniani waliopo kwenye kampeni hiyo.



“On September 25th 2015, 193 world leaders will commit to 17 Global Goals to achieve 3 extraordinary things in the next 15 years. End extreme poverty. Fight inequality & injustice. Fix climate change. The Global Goals for sustainable development could get these things done. In all countries. For all people,” yanasomeka maelezo kwenye tovuti ya Global Goals.