Latest Updates

Jokate aichochea collabo ya Ice Prince na Alikiba

Alikiba ameanza kupata mashavu kupitia mpenzi wake Jokate Mwegelo.


Alikiba, Ice Prince, Jokate na Ne-Yo

Mrembo huyo aliyeyepo jijini Nairobi na muimbaji wa ‘Mwana’, amechochea kufanyika kwa collabo na rapper wa Nigeria, Ice Prince.

Ice na Jokate wanafahamiana kitambo ambapo pamoja kuwa watangazaji wa kipindi cha Top Ten Most cha Channel O, wamefanya wimbo wa pamoja Leo Leo.

Akipost picha akiwa na Ice, Jokate amedai kuwa video ya wimbo wao Leo Leo ipo njiani kuja lakini alimuomba msanii huyo arekodi wimbo na Alikiba na amekubali.

“Forever My G. Ma Nig Fly Boi Choc Boi @iceprincezamani Leo Leo Video Loading. But First I Asked Him To Record A Song With Ali Like Tonite. He’s Like Lets Do This. LoL. #Tanzania #Nigeria #Afrika #Kidoti,” aliandika Jokate.

Mastaa hao walijumuika jana usiku kwenye Coke Studio After Party jijini Nairobi, Kenya.